• Jamii ya wabahai wa Tanzania

Utangulizi wa Imani ya Kibaha’i

Katika historia, Mungu amekuwa akituma kwa binadamu mlolongo wa Waelimishaji watakatifu —wajulikanao kama Wadhihirishaji wa Mungu — ambao mafundisho yao yametoa msingi kwa ajili ya uendelezaji wa ustaarabu. Wadhihirishaji hao hujumuisha Abraham, Krishna, Zoroaster, Moses, Buddha, Jesus, na Muhammad. Bahá’u’lláh, mtume wa sasa miongoni mwa hawa, alieleza kuwa dini za ulimwengu zimekuja kutoka Chanzo kimoja na kwa asili katika mfuatano wa kurasa za dini moja kutoka kwa Mungu.

WaBahá’í huamini kuwa hitaji muhimu linaloikabili binadamu ni utafutaji wa muono wa pamoja wa jamii ya wakati ujao na asili na makusudi ya maisha. Muono kama huo unakunjuka katika maandiko ya Bahá’u’lláh.

Uwepo wa Wa-Baha’i Tanzania

Mnamo 1950 Imani ya Baha’i ilikuja Tanzania. Leo wapo Wa-Baha’i katika takriban maeneo 3000 kila mahali nchini, na zaidi ya halmashauri 150 za Kiroho za Mahali ambazo zinaitwa Mabaraza ya Kiroho ya Mahali. Wa-Baha’i huamini katika elimu ya wote na utokomezaji wa ubaguzi wa aina zote, kama ni wa mbari, kabala, kitaifa, kidini au ya usuli wa kijamii.

Wa-Baha’i huendesha madarasa ya watoto juu ya elimu ya sifa njema na maadili ya mtu; mikutano ya ibada,; na vikundi vya mafunzo kwa ajili ya watu wazima na vijana juu ya mada za kiroho. Wa-Baha’i wa Tanzania wanaendesha Shule ya Sekondari ya Ruaha huko Iringa pamoja na shule nyingine nyingi katika jumuiya za kila mahali nchini.

Acha muono wako uwe ukumbatiao ulimwengu mzima…”

— Bahá’u’lláh

Purpose of our lives

Kusudi la Maisha Yetu

Ufunuo wa Baha’u’llah unathibitisha kuwa kusudi la maisha yetu ni kumjua Mungu na kufikia uwepo Wake. Utambulisho wetu wa kweli ni roho yetu yenye mantiki, ambayo nia yake huru na uwezo wake wa kuelewa hutuwezesha daima kujiboresha wenyewe na jamii yetu...Soma Zaidi

Community Building

Kujenga Jumuiya

“Fikirieni kwa wasiwasi juu mahitaji ya zama tunamoishi, na wekeni maamuzi yenu juu ya matakwa na mahitaji yake.”... Soma Zaidi

Family Life

Maisha ya Familia

“Na juu ya miunganiko yote ni ule kati ya wanadamu, hususan unapotokea kwa sababu ya upendo wa Mungu. Hivyo ndo namna umoja mkuu umefanya kutokea. Hivyi ndo huwekwa msingi wa upendo katika roho”... Soma Zaidi